Genesis 24:10-15

10 aNdipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake, akaondoka, akiwa amechukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimu
Yaani Mesopotamia ya Kaskazini-Magharibi.
na kushika njia kwenda mji wa Nahori.
11 cAkawapigisha ngamia magoti karibu na kisima cha maji nje ya mji, ilikuwa inaelekea jioni, wakati ambapo wanawake wanakuja kuteka maji.

12 dKisha akaomba, “Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nipatie ushindi leo, uonyeshe huruma kwa bwana wangu Ibrahimu. 13Tazama, nimesimama karibu na kisima hiki cha maji, nao binti za watu wa mji huu wanakuja kuteka maji. 14 eBasi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmojawapo, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji,’ naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia.’ Basi na awe ndiye uliyemchagua kwa ajili ya mtumishi wako Isaka. Kwa hili nitajua umemhurumia bwana wangu.”

15 fIkawa kabla hajamaliza kuomba, Rebeka akatokea akiwa na mtungi begani mwake. Alikuwa binti wa Bethueli. Bethueli alikuwa mwana wa Milka aliyekuwa mke wa Nahori ndugu wa Ibrahimu.
Copyright information for SwhKC